Evolution of Marriage – A Tanzania Perspective



Salam wakuu,




Leo nimemkumbuka mwalimu wangu wa somo la siasa enzi hizo kabla ya kubadilishwa na kuitwa uraia. Alikuwa ananiambia katika 'Ndoa' tamaduni mbili zikikutanishwa moja yenye nguvu huimeza iliyodhaifu.

Ili imezwe lazima mmoja aidharau yakwake na kuitukuza ya mwenzie akaniambia wazazi wako na babu zako walishikilia sana tamaduni zao, kuanzia lugha, mila na desturi lakini ninyi mmeanza kuruhusu kumezwa.

Hoja yangu ni ipi haswa.Kwa sasa ndoa zetu zipo mashakani kufikia umri wa ndoa za waliotutangulia hasa wazazi (wenye ndoa) waliishi kwa kuelewa ndoa ililindwa na utamaduni wao wakauenzi

Kwa sasa wanandoa wanaishi nyumba moja kama wako hostel tu na sio familia. Kisa wameruhusu umagharibi kuumeza utamaduni wao.

Mama anadai haki zote za ubaba, na kinyume chake. Hakuna kiwiliwli wote wamekuwa vichwa. Sheria zetu hasa ile ya ndoa ya 1977 nayo bado iliendelea kuegemea kwenye traditional culture. tuna vitu ambavyo hata kama tutaiga umagharibi hatuwezi vipindisha it's norms... mfano: mwanaume haolewi anaoa na ndio mtoa talaka. Hii ina maana gani? Yeye ndio kichwa cha ndoa. Ikitokea akawa Mario ni kosa la kimfumo kichwani mwake.

Siku hizi tuanishi., Ulimwengu wa Kambare kila mtu ana masharubu,mi sishangai sana nnavyoona wanaume tunaoa sio kwa kupenda bali kwa kuridhishwa kwa muda mfupi na vijitabia vya mchumba ili umuoe,na wengi tunaona ufahari sana kutangaza ndoa maana sio mchezo hiyo attention yake ukweni we ndio unakuwa topic+na mchumba ndio kama mlenda na tonge kwa ufupi ndoa siku hizi ni kama hobi tu.Hazina muelekeo wa kimaisha.

Wakati wazee huwa wansaherehekea miaka 50 ya ndoa, siku hizi Utakuta vijana wanasheherekea mwaka mmoja wa ndoa....!

Ndoa za ki Afrika....zimeharibiwa na tamaduni za kigeni na tamthilia.

Kubadilishwa kwa Jando na kuwa Send off(ambazo hazifai).
Upande wa wanaume na wazazi

Yote hayo ni kwa sababu ya kuupoteza utamaduni sasa kama kijana katahiriwa na mama yake kwa nini asiwe marioo? Huwezi kukuta mwanaume alie enda jando na kula kisu bila ganzi akawa marioo

Wanaume wengi nao wamepoteza Sifa za kuwa kichwa cha nyumba. unaishi kwenye nyumba hujui pango ni bei gani, unafungua fridge unatoa beer hujui mke wako ametoa wapi pesa. Hata wife akikwambia anakwenda seminar huna hata nguvu ya kuuliza utakaa muda gani.


Inasikitisha. Tubadilike watanzania. Mmoja mmoja na kama jamii kwa ujumla.

Source: Jamiiiforums

No comments:

Post a Comment